Amesema kuwa hakuna mshindi katika vita vya ushuru.
Rais Xi Ping ameashiria misimamo ya kujichukulia maamuzi ya upande mmoja ya Trump katika kuongeza kiwango cha ushuru wa forodha dhidi ya nchi nyingi duniani na kusema: Kukabiliana na ulimwengu kuna maana ya kujitenga.
Sisitizo la Rais wa China juu ya ulazima wa kukabiliana na maamuzi ya upande mmoja ya Marekani ni katika fremu ya kuongezeka vita vya ushuru kati ya nchi hizi mbili, ambazo ni miongoni mwa mataifa yenye uchumi mkubwa zaidi duniani. Wizara ya Fedha ya China imetangaza kuwa nchi hiyo imeongeza ushuru wa forodha wa asilimia 125 kwa bidhaa zinazoingia nchini humo kutoka Marekani. Awali ushuru wa China kwa bidhaa za Marekani ulikuwa umefikia asilimia 84 na kiwango kipya kilitarajiwa kuanza kutekelezwa jana Jumamosi, Aprili 12. Wizara ya Biashara ya China pia imetangaza kuwa kusitishwa ushuru wa forodha wa Marekani kwa siku 90 dhidi ya baadhi ya nchi waitifaki wa Washington hakubadili ukweli kwamba, Washington inafanya kila iwezalo kunufaika kwa upande mmoja kupitia kuzikandamiza pande nyingine.
Marekani imeongeza ushuru wa asilimia 145 kwa bidhaa zinazotoka China katika kuendeleza vita vyake vya ushuru, lengo likiwa ni kuizidishia China mashinikizo. Nyongeza hizi za ushuru ambazo zimeanzishwa na Rais Donald Trump, zinazidisha hatari ya kuibuka vita vya kibiashara kati ya nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa duniani.
Rais Xi Jin Ping wa China
Ukosoaji wa wazi wa Rais wa China vita vya ushuru wa forodha vya Marekani na sera za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja za Donald Trump unaakisi mtazamo wa Beijing kuhusu hatua za Marekani hasa katika kipindi hiki cha pili cha Rais wa sas wa Marekani. Trump kimsingi anazinyanyasa nchi nyingine duniani na hata kufikia kuwadharau washirika wake wa Ulaya na Magharibi, kama vile Canada. Trump amedhihirisha wazi dhati halisi ya Marekani kwa walimwengu, na huku akidai kuwa Marekani ndiyo nchi yenye uchumi mkubwa na nguvu zaidi duniani na kwamba dola ndiyo sarafu ya kimataifa iliyo bora zaidi, amejikita katika hatua za kimabavu ili kuzitwisha nchi nchi nyingine matakwa yake, sio tu katika uga wa biashara, bali pia katika nyanja nyingine. Pamoja na hayo, hali halisii ya dunia ya leo inaonyesha kudhoofika taratibu Marekani na kuibuka madola mengine hasa China katika uga wa kimataifa. Madola makubwa mahasimu wa Marekani duniani, hasa China na Russia, yanapinga na kukosoa vikali hatua na misimamo ya upande mmoja na hatua za kimabavu za Magharibi na hasa Marekani dhidi ya nchi nyingine. Moscow na Beijing zinaamini kuwa, matukio ya kimataifa na hali halisi ya mfumo wa dunia vinathibitisha kipindi cha mpito kuelekea mfumo wa kambi kadhaa, huku Marekani ikiendeleza mashinikizo yake ili kudumishwa mfumo wa kambi moja ili kuendelea kuidhibiti dunia kkwa kulazimisha malengo na matakwa yake.
Marekani inapinga vikali kuimarishwa mfumo wa kambi kadhaa na inajaribu kudumisha nafasi yake ya kupenda vita kimataifa kwa kutumia mabavu na kulazimisha matakwa yake kwa nchi nyingine; na katika mchakato huo inanufaika na msaada wa baadhi ya washirika wake wa Magharibi. Pamoja na haya yote, ushahidi unaonyesha kutengwa Marekani kwa sababu ya hatua na maamuzi ya upande mmoja na ya mabavu ya Trump na hivyo kupungua kwa nafasi kuu ya Magharibi duniani chini ya uongozi wa Marekani.
Wakati huo huo China inataka mataifa mengine duniani, ukiwemo Umoja wa Ulaya, kuungana ili kukabiliana na sera za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja za Marekani katika kipindi hiki cha pili cha urais wa Trump, hasa kukabiliana na vita vya ushuru na kibiashara. Kuhusu suala hili, Rais Xi Jin Ping wa China ameeleza wazi kwamba: China na Ulaya zinapasa kudumisha ushirikiano wao. Pande mbili lazima zikabiliane na uonevu wa Marekani, lengo likiwa ni kulinda maslahi yao na sheria za kimataifa. Amesisitiza kuwa: Ni jukumu la China na Umoja wa Ulaya kulinda haki na uadilifu wa kimataifa.
342/
Your Comment